Siri

Songs   2025-01-13 03:03:50

Siri

[Barnaba]

Tosa la secret baby

[Vanessa Mdee]

Jamais!

[Barnaba]

Yooo zane valee baby

[Vanessa Mdee]

Yooo zane valee papaaa

[Barnaba]

Treni langu la kutongoza limefunga breki

Na kituo ndo wewe (ndo wewe kipenzi)

Sina mengi mimi, sio mtoto wa mjini

Nimefundwa jandoni kipenzi

[Vanessa Mdee]

Hadithi hadithi uongo njoo

Haya nieleze porojo, mi bado mdogo

Hivi ni juzi ulikuja na maua (yes)

Ulikuwa na barua ila sikuifungua, na na na (why)

[Barnaba]

Ungesoma ndani (why), ungejua vingi (no)

Vile moyo wangu ulivyojawa na vigingi

Wewe una mume (nampenda), na mi n'na mke

Twaweza iba bado wasishituke! (lo!)

[Vanessa Mdee]

Kumbe muhuni

Aku siwezi ku-share penzi nawe

Kasoro yangu nini

Si una mke, yule amekosa nini

Oh uh yeah, oh uh oohh!

[Barnaba]

Kwanza ningekuomba

Kipenzi ukubali

Tutafanya siri ya watu wawili

[Vanessa Mdee]

Utaniponza kwa jambo hili

Hamnaga siri ya watu wawili

[Barnaba]

Kama ukikubali

Nitakupa kagari

Na visalary

Utakuwa bonge la sistaduu

[Vanessa Mdee]

Alinifunza mama

Niogope wavulana

Nikae mbali

Nyie wabaya sana

[Vanessa Mdee]

Kwetu nyumbani

Tumekulia kwenye dini, mmh

Penda wako nyumbani kwanza

Kisha unipende mimi, mmh

(Au uongo baba!)

[Barnaba]

Aaa asante kwa muda wako

Nimependa majibu yako

Hivi nikuulize swali? (niulize nini?)

Anavyotoka mumeo unajua mangapi anafanya?

Ni muhuni (muongo)

Niseme nini (muongo)

Kila kitu (muongo)

Maneno yenu hayakuvuna pendo

[Vanessa Mdee]

Huna jipya (muongo)

Useme nini (muongo)

Maneno yako (muongo)

Kibaya zaidi mke wako akijua

[Vanessa Mdee]

Kumbe muhuni

Aku siwezi ku-share penzi nawe

Kasoro yangu nini

Si una mke, yule amekosa nini (oh no)

Oh yeah, ooh oohh! (ebo!)

[Barnaba]

Ukikubali

Nitakupa kagari

Na visalary

Utakuwa bonge la sistaduu

[Vanessa Mdee]

Alinifunza mama

Niogope wavulana

Nikae mbali

Nyie wabaya sana

[Barnaba]

Kwanza ningekuomba

Kipenzi ukubali

Tutafanya siri ya watu wawili

[Vanessa Mdee]

Utaniponza kwa jambo hili

Hamnaga siri ya watu wawili

[Barnaba]

Kama ukikubali

Nitakupa kagari

Na visalary

Utakuwa bonge la sistaduu

[Vanessa Mdee]

Aliniifunza mama

Niogope wavulana

Nikae mbali

Nyie wabaya sana

See more
Barnaba more
  • country:Tanzania
  • Languages:Swahili, English
  • Genre:
  • Official site:
  • Wiki:
Barnaba Lyrics more
Barnaba Featuring Lyrics more
Excellent Songs recommendation
Popular Songs
Copyright 2023-2025 - www.lyricf.com All Rights Reserved