Kwaru lyrics

Songs   2024-12-28 08:31:58

Kwaru lyrics

Iyo Lizer

Aaah aaah ah

Aaah aaah ah

Ah!

Roho ingekuwa na macho ungejionea

Moyo haufanyi kificho ukigotea

Mimi kipi nisonacho ungeongea

Mwili wangu rochorocho nanyong'onyea

Chungu nilichopika wamepakua, wenzangu

Huruma napokutishwa wamechukua, tonge langu

Na kitabu chetu cha mapenzi

Kurasa umeichanachana

Hazisomeki tena tenzi

Zimepoteza maana

Mpofu moyo wangu

Ulishindwa ona

Hukuandikwa wa kwangu

Limenikaba nalitema

(Kwaru kwakwaru kwaru)

Kachukua kisoda ana ukwangua

(Kwaru kwakwaru kwaru)

Moyo wangu unaumia

(Kwaru kwakwaru kwaru)

Ah! Ye kwa nguvu ana ukwarua

(Kwaru kwakwaru kwaru)

Jamani moyo wangu unaumia

Eh langu tatizo

Nachuna najimaliza

Mi nakesha kumuwaza

Naweweseka lake jina (ooh jina)

Oh! Basi kwa unyonge

Najikaza niache kulia

Mana kwake bahati sina (ooh sina)

Maumivu ameipora furaha yangu

Oooh amekwenda nayo

Na zangu mbivu zimeniozea

Mmh hasara kwangu

Oooh, yatapita nayo

Mpofu moyo wangu

Ulishindwa ona

Hukuandikwa wa kwangu

Limenikaba nalitema

(Kwaru kwakwaru kwaru)

Kachukua kisoda ana ukwangua

(Kwaru kwakwaru kwaru)

Moyo wangu unaumia

(Kwaru kwakwaru kwaru)

Ah! Ye kwa nguvu ana ukwarua

(Kwaru kwakwaru kwaru)

Jamani moyo wangu unaumia

(Wasafi!)

  • Artist:Zuchu
  • Album:I Am Zuchu (2020)
See more
Zuchu more
  • country:Tanzania
  • Languages:Swahili, English
  • Genre:
  • Official site:https://www.instagram.com/officialzuchu/
  • Wiki:https://en.wikipedia.org/wiki/Zuchu?wprov=sfti1
Zuchu Lyrics more
Zuchu Featuring Lyrics more
Excellent Songs recommendation
Popular Songs
Copyright 2023-2024 - www.lyricf.com All Rights Reserved