Si Rahisi lyrics

Songs   2024-07-07 04:49:54

Si Rahisi lyrics

Tarara tarara tara

Ndoto niote eti mimi napepea

Maombi mniombe muziki nizidi bombea

Hutoweza kurekodi kama huna cha kuwapea

Niuze sura nione kama watainunua

Si rahisi kwenye runinga na redio zote nivume

Si rahisi kwenye twitter waseme kanadia katambe

Si rahisi mablogger chocha huyu ndo mwandishi

Si rahisi, si rahisii

Nilifunga safari eti naanza kuimba

Nikajiona wa kusifiwa kama papa wemba

Ngoma zangu zivuke border mpaka kule pemba

Ujumbe nao usikike kote mpaka na wakamba

Ilinivunja moyo waliponifukuza studio nitoke

Wakanidharau familia ndugu wa toka nitoke

Promoter bandia kunipa show kisha jioni apotee

Producer chocha niimbe lingala, nazali nayo mboote

Si rahisi kwenye runinga na redio zote nivume

Si rahisi kwenye twitter waseme kanadia katambe

Si rahisi mablogger chocha huyu ndo mwandishi

Si rahisi si rahisii

Kwenye industry wanatuchesa,controversy zilete pesa

Eti kanadia naye yule,mara nimetemwa vilevile

Wengine wavume bila talanta

Kwenye picha tako wamekamatwa

Jina tupu walishapata, je huu ni ungwana

Eti muziki kizungumkuti

Ikinishinda niipige buti

Ama nianze kucheza isukuti weeee...

Tena yao beef sijazoeaga

Mi ni mpole wananianzaga

Eti sanaa nianze kuaga

Haya maneno zilizaga we

Si rahisi kwenye runinga na redio zote nivume

Si rahisi kwenye twitter waseme kanadia katambe

Si rahisi mablogger chocha huyu ndo mwandishi

Si rahisi, si rahisii

Ata nikifa leo niwe wa kusifiwa

Niliishi kutamani niwe kama Miriam Makebaaa

Si rahisi nisikike, si rahisi nivume

Si rahisi nikubalike...

Si rahisi kwenye runinga na redio zote nivume

Si rahisi kwenye twitter waseme kanadia katambe

Si rahisi mablogger chocha huyu ndo mwandishi

Si rahisi, si rahisii

Cherie, cherie, si rahisi eeh

Si rahisi eh

See more
Nadia Mukami more
  • country:Kenya
  • Languages:Swahili, English
  • Genre:
  • Official site:
  • Wiki:
Nadia Mukami Lyrics more
Nadia Mukami Featuring Lyrics more
Excellent Songs recommendation
Popular Songs
Copyright 2023-2024 - www.lyricf.com All Rights Reserved