Nimwage Radhi

Songs   2024-12-27 00:21:21

Nimwage Radhi

Alilililiiii...

(Ayo lazer!)

[Harmonize]

Furaha isio kifani, kumpata mwandani

Hakika wamependeza

Ngoma lipo uwanjani, kaibiwa nani

Sa unaachaje kucheza

Hama kweli harusi imefana tena ya kihistoria

Pande zote, baba na mama, naona wanashangilia

Ila sitaki kua mnafki, Jumba bovu kuniangukia

Nina langu la moyoni, ningependa kuwaambia

Bi harusi, mashoga wakupupia

Hao niwakuwaangalia

Wako wale wahali gani, wanakuja kuchungulia

Uwaombe samahani, uwakomeshe wambea

Eti, wifi umepika nini, na mimi utanigaia

Waambie, wamepika p dagaa, zenye pilipili nyingi

Zakutisha we na mumeo, wao watakimbia

[Harmonize]

Aiiii shemeji

Ndugu yo mumeo, usisikilize ya fulani

Na hii ndio meseji

Sema na mumeo usifuate ya jirani

Kwa furaha niliyo nayo

Niacheni nimwage radhi (alilililiiii)

Mi nataka nimwage radhi (ai yoi yooo)

Niacheni nimwage radhi

Mi nataka nimwage radhi (alilililiiii)

Ng'ombe anapoita ndama, tunasema kua analia

Kupigwa na kulalama, hatujawahi kusikia

Hakika mmependeza

Ninavyomfahamu biharusi, sipati kusimulia

Nimetoka Ruvuma, Mchomori, namtumbo,

Lindi, mtwara mpaka chitohori nimezisikia

Sifa za binti huyu, Mola amemjalia

Binti hapendi majungu, hakika ninawaambia

Ukimuazia viatu na gauni, anakuachia

Bwana harusi tunakupa mke, ukaishi nae vyema nyumbani

Huna kitu usimfiche mwambie, taabani

Ikiwezekana mkakope, mkono uende kinywani

Usimpige mateke, kisingizio kitu fulani

Ooh umefanya nini jana, hakuliki leo ndani

Mtoto bado mteke, usimkomaze Kwa ngumi

Ukimshindwa mrudishe, kwao hajaua huyu

Mumeo akienda kazini, akirudi salimia

Wala usikae chini, chakula kumsukumia

Bali mkaribishe ndani, hali kumjulia

Muulize za kazini, kwa tabasamu muruua

Kisha msindikize bafuni, hata kama anapajua

Halafu wewe tafuta kiti, jikoni kimbilia

Chukua simu yako message, ukimtumia

Mwambie hasilani bila wewe, chakula hakitaingia

[Harmonize]

Eh!

Aiiii shemeji

Ndugu yo mumeo, usisikilize ya fulani

Na hii ndio message

Sema na mumeo usifate ya jirani

Kwa furaha niliyo nayo

Niacheni nimwage radhi (alilililiiii)

Mi nataka nimwage radhi

Niacheni nimwage radhi

Mi nataka nimwage radhi (alilililiiii)

Nawaomba niishie hapa tarishi huwa hafungwi

Naomba nichape lapa, yaliobaki ni ya makungwi

Niliowakera samahani kusema ni jukumu langu

Nawaomba muishi kwa amani hio ndio furaha yangu

[Harmonize]

Mmh ndio ni kama safari tuombeane dua

Atuepushe na shari saa chini ya jua

Aah somo yake mwari, ainuke

Mama yake mwari, ainuke

Baba yake mwari, aunike

Aje kati tuicheze ngoma

Aah kaka yake mwari, ainuke

Dada yake mwari, ainuke

Shangazi yake mwari, ainuke

Aje kati tulicheze ngoma

Niacheni nimwage radhi

Mi nataka nimwage radhi

Niacheni nimwage radhi

Mi nataka nimwage radhi

See more
Mrisho Mpoto more
  • country:Tanzania
  • Languages:Swahili
  • Genre:
  • Official site:
  • Wiki:
Mrisho Mpoto Lyrics more
Excellent Songs recommendation
Popular Songs
Copyright 2023-2024 - www.lyricf.com All Rights Reserved